Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17, raundi ya 11 inaendelea tena leo kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja viwili tofauti nchini.
Vinara wa Ligi hiyo wekundu wa Msimbazi Simba ndo timu pekee mpaka sasa ambayo hajapoteza mchezo wowote wataikaribisha Toto Africa katika dimba la Uhuru.
Mchezo mwingine jijini Mbeya wajela jela Tanzania Prisons wakiwa nyumbani kuwaalika wachana mbao wabishi Mbao FC kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.
Shirikisho la soka Tanzania TFF linasisitiza kwamba Michezo yote ya Dar es Salaam, mfumo wa kuingia utabaki kuwa ni uleule wa kutumia kadi za Selcom kununua tiketi za kielekroniki.
Viingilio kwenye mechi za Uwanja wa Uhuru ni Sh 30,000 kwa Jukwaa Kuu (VIP-A), VIP-B na C Sh 20,000 na mzunguko ni Sh 5,000.
VPL: SIMBA KUENDELEZA REKODI KWA TOTO
Title: VPL: SIMBA KUENDELEZA REKODI KWA TOTO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17, raundi ya 11 inaendelea tena leo kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja viwili tofa...
Post a Comment