Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara inaendelea leo kwa Michezo mitatu kupigwa katika viwanja tofauti nchini.
Mwadui ya Shinyanga itakuwa wenyeji wa vinara wa ligi hiyo Simba kwenye Uwanja wa CCM Kambarage mkoani Shinyanga.
Kikosi cha Simba tayari kipo mjini Shinyanga toka jumatano asubuhi chini ya usimamizi wa kocha,, Joseph Omog.
Akiongea na tawi la Simba Damu Fans, Meneja wa Simba, Mussa Hassan Mgosi amesema kikosi chao kiko imara na wamejiandaa kuhakikisha wanachukua pointi zote sita katika mkoa wa Shinyanga.
Michezo mingine ya ligi itakayopigwa leo ni:
African Lyon dhidi ya Tanzania Prisons katika Uwanja wa Uhuru, Dar es salaam,
Na mchezo mwingine utawakutanisha JKT Ruvu watakaowakaribisha Ndanda ya Mtwara kwenye Uwanja wa Mabatini, Mlandizi mkoani Pwani
About Author
![](http://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhBBwPSGn21ZfCCiWyZcfL-FXYJTW4SwQZvP7HQAXiex_SxOksYyJ11VIzgPc1zjusJbMgGrT-_N3HyLzEqMVbH7-OPCf9KLDKv_lY3-qWVa0V2isQeEn54Ls659HKLlg/s113/12696110_10204088684058001_1642557258_n.jpg)
Advertisement
![](http://3.bp.blogspot.com/-X9HQZE27FAs/U_gMaSsqmjI/AAAAAAAABnk/zlsF7HIstZM/s1600/Untitled-3.png)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment