Kaimu Mwenyekiti wa kamati hiyo Wakili Levocatus Kuuli alisema walioshitakiwa katika upangaji wa matokeo walikuwa 22 huku 8 pekee ndiyo waliokata rufaa
Hukumu hiyo ilikuwa kama ifuatavyo: 1.Abeid Choki ( Kocha msaidizi wa Geita). Ataendelea na kifungo chake cha kutojihusisha na mpira maisha baada ya rufaa yake kugonga mwamba.
2.Denis Dioniz Richard (Golikipa wa Geita) .Ameachiwa huru kutokana na mapungufu yalikuwepo katika vifungu vya sheria za TFF
3.Geita Gold Mining:Wataendelea na adhabu ya kushushwa daraja baada ya kubadilisha vithibitisho katika rufaa yao.
4.Salehe Mang'ola(Mechi kamishna): Ataendelea na kifungo chake cha kutojihusisha na mpira maisha baada ya rufaa yake kugonga mwamba.
5.Fate Remtula ( kiongozi wa mpira Tabora) Ataendelea na kifungo cha kutojihusisha na mpira maisha baada rufaa yake kushindikana.
6.Yusuph Kitumbo ( Mwenyekiti wa mpira mkoa wa Tabora) Ataendelea kutumikia kifungo cha kutojihusisha na mpira maisha a ya rufaa yake kugonga mwamba.
7.Polisi Tabora.Wataendelea kutumikia adhabu ya kushushwa daraja kutokana na rufaa yao kutupiliwa mbali.
8.JKT Oljoro:Adhabu ya kushushwa daraja itaendelea bali watarudishiwa fedha yao ya rufaa shilingi milioni moja kutokana na kanuni kuwa na mapungufu.
Kamati hiyo imetoa siku 10 kuanzia leo kwa warufani kukata rufaa endapo hawakuridhika na hukumu hiyo.
Labels:
Kitaifa
Post a Comment