SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: SINGIDA YAZIDI KULIZAMISHA JAHAZI LA NJOMBE MJI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Singida United imeiweka Njombe Mji mguu sawa kuelekea kushuka daraja msimu huu baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-0 mtanange uliofanyika...
Singida United imeiweka Njombe Mji mguu sawa kuelekea kushuka daraja msimu huu baada ya kukubali kipigo cha mabao 4-0 mtanange uliofanyika uwanja wa Namfua.

Njombe ipo mkiani mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 22 na  imeshuka dimbani mara 27 ikisalia na mechi tatu pekee.

Mshambuliaji Salita Kambale aliifungia Singida bao la kwanza dakika ya 43 baada ya kazi nzuri ya Lubinda Mundia.

Mlinzi Miraji Adam aliifungia Singida bao la pili kwa mkwaju penati ya 59 kabla ya Mundia kuongeza la tatu dakika mbili baadae.

Nahodha Nizar Khalifan aliwapatia wenyeji bao la nne dakika za lala salama baada ya kutoka benchi kuchukua nafasi ya Mudathir Yahya.

Singida imefikisha pointi 41 na kuendelea kubaki nafasi ya tano  baada ya Tanzania Prisons kupata ushindi wa bao moja dhidi ya Lipuli FC.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top