Kocha msaidizi wa timu ya Simba, Masoud Djuma amesema wanazihitaji pointi tatu muhimu katika mchezo wa leo dhidi ya Ndanda FC ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kuchukua ubingwa.
Simba ndio timu pekee ambayo haijafungwa mechi yoyote ya ligi mpaka sasa ikiwa kileleni mwa msimamo na pointi 62 alama 13 mbele ya Azam iliyo nafasi ya pili.
Kocha Masoud amesema wanafahamu kila ligi inapofikia hatua kama hii inakuwa ngumu kwakua kila mchezo unakuwa na umuhimu lakini wamejipanga kuhakikisha wanafanya vizuri.
Raia huyo wa Burundi ameongeza kuwa wanafahamu watapata upinzani mkubwa kutoka kwa Ndanda kutokana na nafasi waliyopo lakini wataingia uwanjani kutafuta pointi tatu.
"Tunahitaji kushinda kila mchezo, kama tutapata pointi tatu leo dhidi ya Ndanda tutakuwa tumebakisha alama mbili kutwaa ubingwa.
"Wachezaji wote wapo katika hali nzuri na morali ipo juu tukiwa hatuna mchezaji yoyote majeruhi kuelekea mechi hii," alisema kocha Masoud.
MASOUD ASEMA POINTI TATU ZA NDANDA NI MUHIMU KWAO
Title: MASOUD ASEMA POINTI TATU ZA NDANDA NI MUHIMU KWAO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kocha msaidizi wa timu ya Simba, Masoud Djuma amesema wanazihitaji pointi tatu muhimu katika mchezo wa leo dhidi ya Ndanda FC ili kujiweka...


Post a Comment