Kikosi cha wachezaji 20 wa timu ya Yanga kitaondoka nchini saa 11 jioni ya leo kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa makundi wa kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya USM Alger siku ya Jumapili.
Kikosi hicho kitaambatana na viongozi 11 pamoja na benchi la ufundi tayari kwa mtanange huo ambao wanatakiwa kushinda ili kujiweka vizuri kwenye msimamo.
Mkuu wa kitengo cha habari na mawasiliano wa Yanga, Dismas Ten amesema maandalizi yote yamekamilika na muda mfupi kutoka sasa kikosi hicho kitapaa kuelekea Algeria.
"Kikosi chetu kitaondoka saa 11 jioni kuelekea Algeria kwa ajli ya mchezo wetu wa kwanza hatua ya makundi dhidi ya USM Alger siku ya Jumapili," alisema Ten.
Mchezo huo utaanza saa 4 usiku kwa saa za hapa nyumbani Tanzania.
NYOTA 20 WA YANGA KUONDOKA JIONI HII KUWAFUATA USM ALGER
Title: NYOTA 20 WA YANGA KUONDOKA JIONI HII KUWAFUATA USM ALGER
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kikosi cha wachezaji 20 wa timu ya Yanga kitaondoka nchini saa 11 jioni ya leo kuelekea Algeria kwa ajili ya mchezo wa kwanza wa makundi w...


Post a Comment