SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: OKWI: NATAKA KUIPA SIMBA UBINGWA UFUNGAJI BORA NI ZIADA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mshambuliji Emmanuel Okwi amesema hafikirii sana kuhusu kuchukua tuzo ya mfungaji bora wa ligi badala yake anataka kuisaidia Simba kutwaa...
Mshambuliji Emmanuel Okwi amesema hafikirii sana kuhusu kuchukua tuzo ya mfungaji bora wa ligi badala yake anataka kuisaidia Simba kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu.

Okwi ndiye kinara wa ufungaji mpaka sasa akicheka na nyavu mara 18 huku akimzidi mabao matano anayemfuata.

Raia huyo amesema kama mshambuliji anapenda kufunga mabao mengi lakini hata ikitokea hafungi hajisikii vibaya kama timu imepata matokeo.

"Nikifunga au nisipofunga kwangu sio kitu kikubwa ninachotaka kukiona ni Simba inatwaa taji la ligi msimu huu.

"Kuwa mfungaji bora wa ligi kwangu jambo la ziada kikubwa ni kushirikiana na wachezaji wenzangu ni kuhakikisha Simba inatwaa ubingwa msimu huu," alisema Okwi.

Mganda huyo ametengeneza uelewano mzuri na nahodha John Bocco na kuunda safu imara ya ushambuliaji ambayo imezalisha mabao 31 kwenye ligi mpaka sasa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top