Droo ya nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya imetoka ambapo mabingwa watetezi Real Madrid imepangwa kucheza na Bayern Munich.
Mchezo wa kwanza utafanyika Arianz Arena kabla ya kukutana Santiago Bernabeu wiki moja baadae.
Real na Bayern ndio timu zinazopewa nafasi kubwa kutwaa taji hilo kutokana na uwezo walio onyesha ukichangiwa na wachezaji walionao.
Nusu fainali ya pili itawakutanisha Majogoo wa Anfield, Liverpool itacheza na AS Roma katika hatua hiyo.
Liverpool imepangwa kuanzia nyumbani Anfield kabla ya mchezo wa marudiano kupigwa jijini Roma wiki mbili baadae.
Katika droo ya Europa Washika bunduki wa Arsenal itacheza Atletico Madrid wakati Salzburg dhidi ya Marseille.
BAYERN MIKONONI MWA REAL, LIVERPOOL KUWAVAA ROMA UCL
Title: BAYERN MIKONONI MWA REAL, LIVERPOOL KUWAVAA ROMA UCL
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Droo ya nusu fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya imetoka ambapo mabingwa watetezi Real Madrid imepangwa kucheza na Bayern...
Post a Comment