Uongozi wa klabu ya
Yanga umekanusha vikali tetesi kuwa nyota wao Obrey Chirwa atajiunga na watani
wao Simba baada ya kumalizika kwa msimu huu.
Raia huyo wa Zambia
amehusishwa kutaka kujiunga na Simba kufuatia wiki iliyopita kocha msaidizi wa
Wekundu hao Masoud Djuma kumwagia sifa mshambuliji huyo.
Mwenyekiti wa kamati
ya usajili wa klabu hiyo, Hussein Nyika amesisitiza kuwa mshambuliaji huyo
ataendelea kusalia na mabingwa hao na kuhusu kujiunga na Simba alisema jambo
hilo halitatokea kamwe.
"Kuhusu Chirwa
kujiunga na Simba hilo suala halipo na halitatokea, Chirwa ni mchezaji wetu na
hataenda popote tutamalizana nae na ataendelea kubaki hapa," alisema Nyika
kwa kujiamini.
Hata hivyo mkataba wa
Chirwa na mabingwa hao utamalizika mwishoni mwa msimu huu hivyo mabingwa hao
wanatakiwa kupambana ili kufanikisha jambo hilo.
Chirwa ndiye kinara wa
ufungaji kwa mabingwa hao mpaka sasa akifunga mabao 11 manne nyuma ya kinara
Emmanuel Okwi.
Post a Comment