SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: KIYOMBO: SIMBA ILITUZIDI UZOEFU
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mshambuliji wa timu ya Mbao FC, Habib Kiyombo amesema moja ya sababu iliyopelekea kupokea kipigo kikubwa cha mabao 5-0 kutoka kwa jana Sim...
Mshambuliji wa timu ya Mbao FC, Habib Kiyombo amesema moja ya sababu iliyopelekea kupokea kipigo kikubwa cha mabao 5-0 kutoka kwa jana Simba ni kuzidiwa uzoefu.

Mbao ilicheza mechi yake ya kwanza tangu kupanda ligi kuu msimu uliopita katika uwanja wa mkuu wa Taifa ambao eneo lake la kuchezea ni kubwa kulinganisha na viwanja vingi zinavyochezewa ligi.

Kiyombo ambaye anakumbukwa kwa kufunga mabao yote mawili katika ushindi dhidi ya Yanga kwenye uwanja wa CCM Kirumba amesema Simba waliwazidi ujanja karibia kila sehemu.

"Simba ilituzidi, walitengeneza nafasi na kuzitumia vizuri ndio maana wamefanikiwa kushinda, hatuwezi kukata tamaa tutajipanga katika michezo ijayo," alisema Kiyombo.

Katika mchezo wa kwanza uliofanyika kwenye Uwanja wa Kirumba timu hizo zilitoka sare ya mabao 2-2.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top