SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: OKWI HASHIKIKI DAR, SIMBA YAIPIGA MKONO MBAO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mshambuliji Emmanuel Okwi ameendeleza moto wake akiwa kwenye ardhi ya Dar es Salaam baada ya kuisaidia Simba kuibuka na ushindi mnono wa m...
Mshambuliji Emmanuel Okwi ameendeleza moto wake akiwa kwenye ardhi ya Dar es Salaam baada ya kuisaidia Simba kuibuka na ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Mbao FC.

Katika ushindi huo Okwi alifunga mabao mawili dakika za 41 kwa mkwaju wa penati na jingine dakika ya 69 huku akitengeneza la kwanza lililofungwa na Shiza Kichuya.

Okwi ameendelea kujichimbia kileleni mwa orodha ya wafungaji akifikisha mabao 16 akifuatiwa na Obrey Chirwa wa Yanga mwenye 11

Katika mchezo huo mabao mengine ya Simba yalifungwa na Erasto Nyoni kwa mpira wa adhabu dakika ya 82 na Nicholas Gyan akifunga la mwisho dakika ya 86 likiwa ndio la kwanza tangu ajiunge na Wekundu hao.

Simba imefikisha pointi 45 alama nane mbele ya Yanga ambao keshokutwa Jumatano itakutana na Ndanda FC katika uwanja wa Nangwanda Sijaona.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top