SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: BOCCO AKABIDHIWA TUZO YAKE YA MWEZI JANUARI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mshambuliaji John Bocco wa timu ya Simba amekabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2017/18 kwa mwezi Januari...
Mshambuliaji John Bocco wa timu ya Simba amekabidhiwa tuzo yake ya mchezaji bora wa ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2017/18 kwa mwezi Januari na wadhamini wa ligi hiyo.

Kwenye kinyang'anyiro hicho Bocco aliwashinda nyota mwenzake wa Simba  Emmanuel Okwi na kiungo wa Mwadui FC Awesu Awesu

Nahodha huyo amekabidhiwa hundi ya sh milioni moja, ngao na kisimbuzi cha Azam TV kama sehemu ya zawadi hiyo.

Bocco alikabidhiwa zawadi hizo muda mfupi kabla ya kuanza mchezo wa ligi kuu kati ya Simba dhidi ya Mbao FC uliofanyika kwenye uwanja wa Taifa.

Nyota huyo wa zamani wa Azam FC amekuwa mchezaji wa pili wa Simba kupata tuzo hiyo baada ya Okwi aliyepata mwezi Agosti.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top