Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom timu ya Yanga imetumia dakika 10 za mwisho kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Reha FC katika mchezo wa kombe la FA uliofanyika uwanja wa Uhuru.
Licha ya kutengeneza nafasi na kushambulia muda mwingi wa mchezo lakini iliwabidi wasubiri mpaka dakika ya 82 kupata bao la kwanza lililofungwa na Pius Buswita.
Amiss Tambwe alifunga la pili dakika ya 85 kwa kichwa baada ya kukosekana mawasiliano baina ya walinzi na mlinda mlango wao.
Reha ambayo inashiriki ligi daraja la pili ikifundishwa na mlinda mlango wa zamani wa Yanga, Ivo Mapunda ilionyesha upinzani mkubwa lakini walizidiwa maarifa hasa kipindi cha pili.
Yanga inakuwa miongoni mwa timu 32 zilizofuzu hatua ya tatu ya michuano hiyo ambayo droo yake itafanyika siku chache zijazo.
YANGA YATUMIA DAKIKA 10 KUIUA REHA
Title: YANGA YATUMIA DAKIKA 10 KUIUA REHA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Vodacom timu ya Yanga imetumia dakika 10 za mwisho kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Reha FC katika mc...
Post a Comment