SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: AZAM YAIPIGA MKWARA MZITO STAND UNITED
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Baada ya kufuzu michuano ya kombe la FA kwa kuifunga Area C mabao 4-0 jana, Azam FC imehamisha nguvu kwa Stand United katika mchezo wa lig...
Baada ya kufuzu michuano ya kombe la FA kwa kuifunga Area C mabao 4-0 jana, Azam FC imehamisha nguvu kwa Stand United katika mchezo wa ligi utakaofanyika wikiendi ijayo.

Azam itashuka dimbani kwenye uwanja wake wa Azam Complex kuwakaribisha wapiga debe hao Disemba 30 ambapo wamejidhatiti kubaki na alama zote tatu.

Msemaji wa klabu hiyo, Jaffer Idd amesema wameelekeza nguvu kwenye mchezo huo huku wakijipanga kuhakikisha wanashinda ili kujiweka kwenye mazingira mazuri ya ligi.

"Tumemaliza mchezo wetu dhidi ya Area C na maandalizi ya mechi ya Stand yameanza mara moja kikubwa ni kuhakikisha tunashinda pia mchezo huo," alisema Jaffer.

Azam inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 23 sawa na Simba ikizidiwa mabao yakufunga pekee.

Jaffer amesema baada ya mchezo huo timu itasafiri kuelekea visiwani Zanzibar kwa ajili ya michuano ya Mapinduzi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top