Msajili wa vyama vya michezo na vilabu (kushoto) akimwakilisha waziri wa habari, sanaa, utamaduni na michezo. Kulia ni kaimu rais wa klabu ya Simba |
Mwenyekiti wa kamati ya Zabuni Jaji mtaafu Thomas Mihayo akiwasalimu wanachama wa Simba kabla ya kumtangaza mshindi wa zabuni ya uwekezaji ndani ya klabu ya Simba |
Makamu wa rais wa Shirikisho la mpira Tanzania Michael Richard Wambura akiliwakilisha shirikisho hilo katika mkutano wa Simba |
Kulia ni mwanachama wa Simba, Bi. Hindu aliyekuwa akipinga kwa nguvu zote mabadiliko katika klabu hiyo akifuatilia kwa makini mkutano wa kumtangaza mshindi wa zabuni |
Wanachama wa Simba walilipuka kwa shangwe mara baada ya kutangaziwa jina la mshindi wa zabuni ya uwekezaji ndani ya klabu yao. |
Msemaji wa Simba Haji Manara (mwenye suti kushoto) akimkaribisha ukumbini mfanyabiashara Mohammed Dewji (aliyepunga mikono miwili) mara baada ya jina lake kutangazwa mshindi wa zabuni |
Mohammed Dewji 'MO' akiwasalimu wanachama wa Simba mara tu alipotangazwa mshindi wa zabuni na kuingia ukumbini |
MO akisalimiana na kaimu rais wa Simba Salim Abdallah 'TRY AGAIN' |
MO akisalimiana na katibu wa kamati ya zabuni Bi. Brenda Mrema |
Mohammed Dewji akiwashukuru wanachama kabla ya kukaa mara baada ya kuingia ukumbini |
MO akiwa amekaa katikati ya mgeni rasmi kulia na kushoto ni mwenyekiti wa kamati ya zabuni |
MO Dewji alipokuwa akiwaeleza wanachama mipango ya muda mrefu na mfupi ndani ya klabu ya Simba mara baada ya kushinda zabuni |
MO akipeleka ujumbe kwa wachezaji watakaoichezea klabu ya Simba kutambua thamani kubwa ya kuvaa jezi ya timu hiyo uwanjani |
Mo akipeana mikono na mgeni rasmi baada ya kuelezea mipango yake ndani ya Simba |
Mwanachama wa Simba akiserebuka baada ya kusikia mipango ya muda mrefu na mfupi kutoka kwa mwekezaji MO |
Ilikuwa ni shangwe tupu ndani ya ukumbi wa Mwl Nyerere, wanasimba wakifurahia mipango ya mwekezaji katika timu yao |
Salim Abdallah "Try Again" kaimu rais wa Simba aliyeongoza kwa uweledi wa hali juu mchakato wa mabadiliko katika klabu ya Simba |
MO akionekana mwenye furaha kubwa mara baada ya mchakato wa uwekezaji kukamilika kwa zaidi ya asilimia 99.99 |
Makamu wa rais wa TFF, Mwenyekiti wa kamati ya zabuni na mshindi wa zabuni |
Makamu wa rais wa TFF akiteta jambo na Mo wakati mkutano ukielekea kuisha |
Jaji Mtaafu Thomas Mihayo akifurahia jambo na Mohammed Dewji |
Mwanasheria Msomi na aliyewahi kuwa katibu mkuu wa Simba Evodius Mtawala akifafanua hatua zinazofuata baada ya kutangazwa mshindi wa zabuni ya uwekezaji katika klabu ya Simba |
RUBUDANI KWENDA KWA MBELE.
ReplyDelete