Timu ya Singida United itatumia uwanja wake wa Namfua kwa mara ya kwanza katika mechi za ligi kwa kuikaribisha Yanga jioni ya leo baada ya kukamilika kwa ukarabati wake.
Singida ambayo imepanda ligi msimu huu ilikuwa ikitumia uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma kama uwanja wake wa nyumbani lakini leo wana rejea Namfua kutokana na bodi ya ligi (TPLB) kuthibitisha kuwa uwanja huo upo tayari kuchezea mechi za ligi.
Timu hiyo inayonolewa na kocha wa zamani wa Yanga Mholanzi Hans van Pluijm imefanya usajili mkubwa kwa kuleta wachezaji saba wa kigeni ambao wanacheza timu zao za taifa, ipo nafasi ya sita ikiwa na pointi 13 katika msimamo wa ligi.
Timu za Yanga, Azam na Mtibwa Sugar zenye pointi 16, zina nafasi ya kukaa kileleni mwa msimamo kama zitashinda mechi zao za leo kutokana na vinara Simba kushuka dimbani kesho.
Kagera Sugar ambayo ilipata ushindi wake wa kwanza wiki iliyopita na kuondoka mkiani mwa msimamo itakuwa kwenye uwanja Kaitaba kuikaribisha Tanzania Prisons.
Ruvu Shooting ambao ndio wako mkiani watakuwa katika uwanja wa Azam Complex kumenyana na Azam usiku wa leo.
Ratiba kamili ya mechi za VPL Jumamosi ya leo
Singida United vs Yanga
Kagera Sugar vs Tanzania Prisons
Njombe Mji vs Mbao FC
Ndanda FC vs Mtibwa Sugar
Azam FC vs Ruvu Shooting
SINGIDA KUZINDUA NAMFUA KWA USHINDI MBELE YA YANGA?
Title: SINGIDA KUZINDUA NAMFUA KWA USHINDI MBELE YA YANGA?
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Singida United itatumia uwanja wake wa Namfua kwa mara ya kwanza katika mechi za ligi kwa kuikaribisha Yanga jioni ya leo baada ya...
Post a Comment