Kiungo Aaron Ramsey wa Arsenal anaamini wamepitia kipindi kigumu baada ya kumalizika kwa dirisha la usajili mwezi Agosti kwakuwa hawakuwa na mwenendo mzuri.
Ramsey na timu yake ya Arsenal kesho watakutana na vinara wa ligi hiyo Manchester City ambao wako kwenye kiwango bora chini ya kocha Pep Guardiola kwenye uwanja wa Etihad.
Arsenal ilifungwa na Stoke City kabla ya kupokea kichapo kikubwa cha mabao 4-0 kutoka kwa Liverpool mwezi Agosti kipindi ambacho wachezaji wao nyota Alexis Sanchez na Mesut Ozil wakiwa hawajui mustakabali wao klabuni hapo.
Ramsey amesema, Alex Oxlade-Chamberlain alijiunga na Liverpool kwa ada ya pauni 35 milioni siku ya mwisho ya usajili huku Arsenal ikimaliza mwezi huo kwa vipigo mfululizo.
Kiungo huyo raia Wales amesema wamepoteza mchezo mmoja katika mashindano yote katika mwezi Septemba ambapo amekiri kuwa wamejifunza kitu kupitia kipigo kutoka wa Liverpool huku akisifu kiwango walicho onyesha katika mechi ya sare ya bila kufungana dhidi Chelsea.
"Kilikuwa ni kipindi kigumu kwetu kama timu, hatukuwa sawa sidhani kama ilikuwa ni moja ya sababu ya kutofanya vizuri.
"Tulijifunza kutoka pale, tulienda Stamford bridge na kuonyesha kiwango safi labda tulikosa tu bahati ya kuingiza mpira wavuni," alisema Ramsey.
RAMSEY: AGOSTI ILIKUWA NA 'GUNDU' KWETU
Title: RAMSEY: AGOSTI ILIKUWA NA 'GUNDU' KWETU
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kiungo Aaron Ramsey wa Arsenal anaamini wamepitia kipindi kigumu baada ya kumalizika kwa dirisha la usajili mwezi Agosti kwakuwa hawakuwa...
Post a Comment