Ligi Ndogo ya Wanawake sasa
itaanza rasmi Septemba 30, 2017 katika Kituo cha Dar es Salaam badala ya
Septemba 22, mwaka huu.
Wakati tayari timu zimepewa taarifa
rasmi juu ya tarehe hiyo mpya, lakini kwa taarifa hii, timu zilizoko mikoani
zisianze safari kwa sasa.
Kupelekwa mbele kwa tarahe husika kumetokana
na taratibu za mwisho za usajili ambako sasa timu bingwa wa mkoa inayotambuliwa
na mkoa, lazima itimize masharti matatu.
Kwanza; Ni kuthibitisha kushiriki kucheza ligi
ndogo kabla ya Septemba 25, mwaka huu.
Pili; kuthibitisha kama imesajiliwa kwa
Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo (Klabu iwe na hati ya usajili) na tatu
kuwasilisha majina ya wachezaji wake iliyowasajili kwa .
Kama kuna timu bingwa kwa mujibu wa mkoa, na
tayari ina majina ya wachezaji iliyowasajili msimu huu, lakini haina hati ya
usajili kutoka kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya mchezo, basi klabu hiyo
itakosa sifa ya kushiriki.
Sharti kubwa ni kwamba timu au klabu hiyo
lazima iwe imesajiliwa kwa Msajili wa Klabu na Vyama vya Michezo. Ndio
utaratibu.
Ligi Ndogo inachezwa ili kupata timu mbili
zitakazopanda daraja kucheza Ligi Kuu ya Wanawake Tanzania Bara msimu wa
2017/18 baada ya timu mbili kushuka msimu wa 2016/17.
Ligi ya msimu ulipita bingwa ni Mlandizi
Queens ya Pwani wakati zilizoshuka daraja ni Viva Queens ya Mtwara na Victoria
Queens ya Kagera.


Post a Comment