Uongozi wa timu ya soka ya Simba SC umesema mchezaji wao
Shizya Kichuya yuko tayari kwajili ya mchezo wao wa Jumapili ambapo timu hiyo
itavaana na Stand united mkoani Shinyanga katika uwanja wa CCM Kambarage.
Akizungumza katika mahojiano maalumu Mratibu wa klabu ya Simba SC Abass Suleiman alisema mchezaji wao Shiza
Kichuya yuko njema na anatarajia kucheza dhidi ya Stand united.
Abass alisema Kichuya alianza mazoezi tokea siku
ya Jumatatu na siku za Jumanne na Jana,Kichuya amekuwa akifanya mazoezi na
wenzake.
Mratibu huyo alisema timu yao ilicheza mchezo wa
kirafiki mkoani Tabora ambapo timu hiyo ilipata sare ya bila kufungana dhidi ya
Mirambo.
Akielezea mchezo huo,Abass alisema timu yao
ilitumia mchezo huo kama sehemu ya kurekebisha makosa yao yaliojitokeza dhidi
ya mchezo wao na Mbao FC.
Akielezea kuhusu hali za wachezaji Said
Mohamed’Nduda’ na Shomari Kapombe,Abass alisema Ndunda ataondoka nchini
Jumapili kwenda India kwajili ya matibabu.
Abass alisema Nduda atakuwa India siku 4 za matibabu
kisha atarejea nchini na baada ya wiki 4,kipa huyo atanza mazoezi.
Kwa upande wa hali ya mchezaji Kapombe,Abass
alisema Kapombe ameanza mazoezi mepesi na anatarajia kujiunga na timu yao
itakaporejea Dar-es-salaam
Habari njema. Sc nguvu moja.
ReplyDelete