Uongozi wa
Iringa football academy unapenda kutoa taarifa juu ya vijana wao wanne kuitwa
katika majaribio katika timu ya taifa ya vijana (u17) vijana wawili walichujwa
na wawili waliweza kuendelea na mazoezi pale uwanja wa karume chini ya kocha
mkuu wa vijana Kim Poulsen
Iringa football academy inatoa shukrani za dhati kwa
uongozi wa TFF pamoja na benchi zima la ufundi kwa kutoa nafasi ya kupeleka
vijana wao, pia inatoa shukrani za dhati kwa wazazi na walezi kwa kutoa ruhusa
kwa vijana wao kwenda kuonesha vipaji vyao ili kulipigania taifa leo.
Kambi ya viajana hao ilikuwa ya mwezi mmoja na
imevunjwa rasmi juzi
Kikosi hiko cha vijana kinaandaliwa kwa ajili ya
mashindano ya u17 yatakayofanyika mwaka 2019 Tanzania ndio mwenyeji wa
mashindano hayo


Post a Comment