Mwamuzi wa kimataifa, Elly Sasii atakuwa mwamuzi katika
mchezo wa kirafiki kati ya Taifa Stars ya Tanzania na Zebras ‘Pundamilia’ ya
Botswana utakaofanyika kesho Jumamosi Septemba 2, mwaka huu.
Katika mchezo huo wa kirafiki wa
kimataifa utakaofanyika kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam waamuzi wasaidizi
watakuwa Soud Lillah (Line 1) na Frank Komba (Line 2) wakati mwamuzi wa akiba
(Forth Official) atakuwa Israel Nkongo.
Mchezo huo utaanza saa 10.00
jioni unaochezwa chini utaratibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira
wa Miguu (FIFA) ambako Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limepanga
Watazamaji waingie uwanjani kwa kiingilio cha Sh 10,000 kwa Jukwaa Kuu na Sh
5,000 kwa mzunguko.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum
Mayanga leo Ijumaa amezungumza na wanahabari kwenye Ukumbi wa Hosteli ya TFF,
Karume jijini Dar es Salaam ambako amethibitisha kwamba kikosi chake kiko imara
kwa mapambano.
Kwa upande wa Kocha wa Botswana,
David Bright amesema yeye ni kocha mpya na amejitahidi kuteua timu mpya yenye
mchanganyiko wa vijana na wazoefu aliokuja nao kuwajaribu kwa nyota wa
Kitanzania.
Taifa Stars iko kambini na nyota
wake akiwamo Nahodha Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Elias Maguli (Dhofar
FC/Oman), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Hamis Abdallah (Sony
Sugar/Kenya),Farid Mussa (CD Tenerif/Hispania) na Simon Msuva (Difaa El Jadidah
ya Morocco).
Wengine ambao wako kambini Hoteli
ya Sea Scape iliyoko Kunduchi, Dar es Salaam ni makipa Aishi Manula (Simba SC),
Mwadini Ally (Azam FC) na Ramadhani Kabwili (Young Africans).
Pia wamo Walinzi ni Gadiel
Michael (Young Africans), Boniphas Maganga (Mbao FC), Kelvin Yondani (Young
Africans), Salim Mbonde (Simba SC) na Erasto Nyoni (Simba SC).
Viungo ni Himid Mao - Nahodha
Msaidizi (Azam FC), Mzamiru Yassin (Simba SC), Said Ndemla (Simba SC), Shiza
Kichuya (Simba SC), wakati Washambuliaji ni Raphael Daud (Young Africans),
Kelvin Sabato (Azam FC) na Emmanuel Martin (Young Africans).
Post a Comment