Timu ya soka ya Simba wameanza ligi kuu Tanzania Bara kwa ushindi mnono wa mabao 7-0 dhidi ya maafande wa Ruvu Shooting leo katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Emmanuel Okwi aliweka rekodi mpya ya kufunga magoli matatu ndani ya kipindi cha kwanza katika ligi kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Mpaka mapumziko Simba walikuwa mbele kwa mabao 5-0, magoli matatu yakiwekwa kambani na Mganda Emmanuel Okwi aliyerejea Msimbazi kwa mara ya tatu msimu huu, huku Juma Luizio na Shiza Ramadhan Kichuya wakifunga goli moja moja kila mmoja, wote wawili wakimalizia kazi nzuri za beki wa kushoto aliyetua Simba msimu huu akitoa kwa waoka mikate Azam FC Erasto Edward Nyoni.
Kipindi cha Pili kilianza kwa kasi na Emmanuel Okwi tena akaandika goli la sita kwa Simba na la nne kwake kwa kichwa akiunganisha krosi safi toka kwa kiungo Said Khamis Ndemla aliyeingia kipindi cha pili kuchukua nafasi ya Mzamiru Yassin. Alikuwa ni Said Khamis Ndemla tena alimuwekea pasi ndefu Erasto Nyoni aliyeunganisha kwa guu la kushoto na kukwamisha mpira wavuni kuhitimisha goli la saba kwa wekundu wa Msimbazi
Simba walifanya mabadiliko ya mapema baada ya nyota wake Haruna Niyonzima kuumia kipindi cha kwanza na nafasi yake kuchukuliwa na Mohamed Ibrahim
Kipindi cha Pili Simba walimuingiza Juuko Murshid na Said Khamis Ndemla kuchukua nafasi za nahodha Method Mwanjali na Mzamiru Yassin
Mechi ijayo Simba watacheza na Azam FC
OKWI AANZA LIGI NA HATRIKI, MNYAMA AKIUA SABA
Title: OKWI AANZA LIGI NA HATRIKI, MNYAMA AKIUA SABA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya soka ya Simba wameanza ligi kuu Tanzania Bara kwa ushindi mnono wa mabao 7-0 dhidi ya maafande wa Ruvu Shooting leo katika uwanja ...


Post a Comment