Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara, timu ya Yanga Leo imepata ushindi muhimu mbele ya Wauza ice cream wa Azam baada ya kuifunga goli moja kwa bila.
Goli La yanga lilifungwa na mshambuliaji wake raia wa Zambia Obrey Chirwa katika dakika ya 70 baada ya mabeki wa Azam kutegeana kuokoa mpira mrefu uliopigwa na Haruna Niyonzima na kumpa nafasi Chirwa kutulia kisha kufumua shuti kali lililomshinda golikipa wa Azam Aishi Manula na kuhesabu goli la kwanza na la pekee katika mechi hiyo.
Azam itabidi wajilaumu wenyewe kwani kipindi cha kwanza walipata nafasi kadhaa lakini walishindwa kuzitumia, ambapo Yanga walikuwa wakipoteana Mara kwa Mara, kipindi hicho cha kwanza kilishuhudia pia Yanga wakimpoteza kiungo wao mkabaji Justice Zulu aliyeumia na nafasi yake kuchukuliwa na Anthony Martin.
Kipindi cha pili Yanga ilibadilika na kulisakama lango la Azam Mara kwa Mara, lakini hadi dakika 90 za mchezo huo zinamalizika, Yanga 1 na Azam 0.
Kwa matokeo hayo sasa Yanga wamefikisha point 56 na kuishusha Simba iliyokuwa kileleni kwa point 55 lakini ikiwa na nafasi ya kurudi kileleni kesho ikiwa itaifunga Kagera Sugar huko kwenye uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.
YANGA YAKAA KILELENI MWA MSIMAMO LIGI KUU BARA
Title: YANGA YAKAA KILELENI MWA MSIMAMO LIGI KUU BARA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara, timu ya Yanga Leo imepata ushindi muhimu mbele ya Wauza ice cream wa Azam baada ya ku...
Post a Comment