SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: NIYONZIMA : HATUWAHOFII MASHABIKI WA SIMBA KIMATAIFA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kiungo wa kimataifa wa Timu ya soka ya Yanga SC Haruna Niyonzima amewashangaa wale wote wanaotaka vijana hao wa Jangwani wahamishie mechi...

Kiungo wa kimataifa wa Timu ya soka ya Yanga SC Haruna Niyonzima amewashangaa wale wote wanaotaka vijana hao wa Jangwani wahamishie mechi zao za kimataifa kwenye uwanja wa CCM Kirumba Mwanza, ili kuwakimbia mashabiki wa Simba.

Akiongea leo Niyonzima alisema  haoni sababu ya kuhama  uwanja wa Taifa kwasababu hao Simba hata huko Mwanza wapo

"Hao Simba wanaweza kuja hata mpaka nje ya nchi mpira wa sasa ni mipango na maandalizi tu, ukijipanga na kujiandaa vizuri unashinda popote, kwangu mimi sioni sababu ya kuhama uwanja wa taifa na sidhani kwamba hata kocha wetu alishauri hicho kitu" alisema Niyonzima.

Wiki mbili zilizopita kulikuwa na taarifa kwamba viongozi wa Yanga wanafikiria kuhamishia mechi zake za kimataifa kanda ya ziwa kwenye uwanja wa CCM Kirumba ili kuwakwepa Mashabiki wa Simba wanaozishangilia timu ngeni zinapokuja kucheza mechi za kimataifa kwenye uwanja wa Taifa dhidi ya Yanga. Lakini juzi Jumatano SDFSPORT ilimnukuu mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga Salum Mkemi akisema mechi za vijana hao wa Jangwani zitachezwa hapa hapa Dar es salaam kwenye dimba  la Taifa.

Mwishoni mwa wiki ijayo Yanga watacheza mechi yao ya kuwania kufuzu hatua ya makundi katika kombe LA shirikisho dhidi ya MC Alger ya Algeria.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top