SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: SIMBA YAPUMULIA UBINGWA KAMATI YAIPA POINTI ZA KAGERA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kuikata Klabu ya Kagera Sugar  alama tatu pamoja na magoli matatu baada ya kukiuka kanuni za...
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza kuikata Klabu ya Kagera Sugar  alama tatu pamoja na magoli matatu baada ya kukiuka kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom kwa kumchezesha mchezaji ambaye haruhusiwi kucheza.

Akizungumzia hatua hiyo, Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas Mapunda amesema Kagera Sugar ilimchezesha beki wake Mohamed Fakhi akiwa na kadi tatu za njano katika mchezo wa ligi kuu ya dhidi ya Simba kitendo ambacho ni tofauti na kanuni.

Amesema kutokana na kanuni na sheria za ligi kuu, timu ambayo inafanya kitendo hicho inatakiwa kukatwa alama tatu na magoli matatu hivyo na Kagera Sugar imechukuliwa hatua hiyo ambayo itakuwa ni funzo kwa vilabu vingine.

“Kagera walimchezesha Fakhi katika mchezo uliochezwa Aprili, 2 katika uwanja wa kaitaba, Mjini Kagera dhidi ya Simba ni kinyume na kanuni na wanatakiwa kuadhibiwa kwa kunyanganywa alama tatu na magoli matatu,” amesema Mapunda.

Baada ya kukatwa alama sasa Kagera Sugar, Yanga wameshushwa nafasi moja kutoka nafasi ya kwanza hadi ya Pili na Simba Kurudi kileleni kwa ligi Kuu kwa Point 61 huku yanga akibaki na pointi 56

About Author

Advertisement

Post a Comment

  1. Ahsanteh Mola kwa kuijaalia kamati Haki imetendeka.

    ReplyDelete
  2. We deserved it....sasa bampa to bampa hadi ubingwa

    ReplyDelete
  3. Mwaka wa ubingwa huuu....Simba Nguvu moja, we surely deserve it

    ReplyDelete
  4. Simba nguvu moja sasa nguvu zetu zote tunaziamishia mwanza kwa Toto mungu jaalia simba

    ReplyDelete

 
Top