Mchezaji wa timu ya Kagera Sugar FC, Mbaraka Yusuph Abeid
amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Machi
kwa msimu wa 2016/2017.
Mbaraka aliwashinda wachezaji Abubakar Salum wa Azam FC na Kenny Ally
wa Mbeya City kutokana na kuonyesha kiwango cha hali ya juu, hivyo
kuisadia timu yake kupata matokeo mazuri.
Katika mwezi ho ilichezwa raundi moja tu na Mbaraka ambaye alicheza
kwa dakika zote 90 aliisaidia timu yake kukusanya pointi zote tatu
zilizoifanya timu yake kubaki katika nafasi ya nne (4) katika msimamo wa
ligi kwa mwezi huo.
Katika mchezo huo mmoja, Mshambuliaji huyo alifunga goli moja, na
alionyesha nidhamu ya hali ya juu, hivyo kutopata onyo lolote la kadi.
Kwa kushinda tuzo hiyo, Mbaraka atazawadiwa kitita cha sh. 1,000,000
(milioni moja) kutoka kwa wadhamini wa Ligi hiyo, kampuni ya Vodacom
Tanzania PLC.
MBARAKA YUSUPH MCHEZAJI BORA MACHI
Title: MBARAKA YUSUPH MCHEZAJI BORA MACHI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mchezaji wa timu ya Kagera Sugar FC, Mbaraka Yusuph Abeid amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Ligi Kuu ya Vodacom wa mwezi Machi kwa msim...
Post a Comment