Shaban Idd aliipatia Azam bao la kwanza dakika ya 13 baada ya kupokea pasi ndefu kutoka Abubakar Salum bao lililodumu kwa dakika mbili kwani William Lucian aliisawazishia Ndanda kwa shuti kali baada ya mlinda mlango Aishi Manula kupangua shuti lililopigwa na Kigi Makasi kabla ya kumkuta mchezaji huyo aliyekulia kwenye timu ya vijana ya Simba.
Beki Yakub Mohammed wa Azam alishindwa kuendelea na mchezo baada ya kutolewa dakika ya 21 kufuatia kuumizwa usoni na kiungo Salum Telela ambapo kocha Aristica Cioba alimuingiza David Mwantika kuchukua nafasi ya raia huyo wa Ghana.
Dakika kumi baadae mlinda mlango wa Ndanda Jeremiah Kisubi alishindwa pia kuendelea baada ya kuumia na nafasi yake ikachuchukuliwa na Wilbert Mweta.
Shaban tena aliipatia Azam bao la pili dakika ya 45 kwa aina ile ile ya bao la kwanza baada kumalizia mpira mrefu uliopigwa na beki Daniel Amoah kabla ya Samwel Afful kuugusa na kumkuta kinda huyo anayekuja kwa kasi katika medani ya soka nchini.
Ramadhan Singano aliifungia Azam bao la tatu dakika ya 45 kipindi cha pili baada ya kupiga mpira wa krosi ulioingia wavuni moja kwa moja akitokea upande wa kushoto.
Azam imeungana na timu za Simba na Mbao FC ambazo zilifuzu hatua hiyo mwezi uliopita.
Post a Comment