SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: MALINZI AITISHIA SIMBA KESHO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Msemaji wa Timu ya Mbao fc Chrisant Malinzi amewaonya Simba  kwamba wajipange vizuri kwa mchezo utakao wakutanisha kesho katika uwanja wa ...
Msemaji wa Timu ya Mbao fc Chrisant Malinzi amewaonya Simba  kwamba wajipange vizuri kwa mchezo utakao wakutanisha kesho katika uwanja wa CCM Kirumba kwa sababu vijana wake hawana huruma na Timu yoyote kwa sasa.

Malinzi ameiambia sdfblog kwamba kwa sasa Timu imejipanga kushinda michezo yote iliyo baki na kuanzia mchezo wa kesho tunawaonya simba kwamba wasitarajie mteremko kwasababu tunataka tubaki ligi kuu.

"Tuna waheshimu simba tunajua wapo kwenye mbio za ubingwa lakini sisi hatuangalii hilo kwasababu na sisi tunataka tukae kwenye nafasi nzuri tubaki ligi kuu, Naamini mchezo wa kesho utakua mgumu kuliko hata ule wa kwanza tuliocheza nao Dar es salaam"alisema.

Wakati simba kesho wakishuka uwanjani kusaka pointi 3 ili warudishe matumaini ya kubeba ubingwa msimu huu, Wenyeji wao Mbao fc wanaonekana nao wanataka pointi 3 ili wajihakikishie kubaki ligi kuu.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top