Timu ya Yanga imeibuka na usindi wa bao moja dhidi ya MC Alger katika mchezo wa kombe la Shirikiso Afrika uliofanyika kwenye uwanja wa taifa Dar es Salaam.
Kiungo Mzimbabwe Thaban Kamusoko alifunga bao hilo pekee dakika ya 60 kufuatia kugongeana na Chirwa ndani ya eneo la hatari la Alger.
Yanga itabidi wajilaumu wenyewe kwani walikosa nafasi za wazi za kufunga ambazo zingewafanya kuondoka na mtaji mzuri wa mabao ambayo yangewafanya kuwa kwenye nafasi nzuri ya kusonga mbele katika mchezo wa marudioano wiki ijayo.
Obrey Chirwa alipoteza nafasi mbili za wazi kipindi cha kwanza huku Kamusoko pia akipoteza nafasi mbili ambazo kama wangezitumia vizuri wangepata ushindi mnono.
Kocha George Lwandamina anapaswa kufanya marekebisho kwenye safu ya ulinzi kutokana na kufanya makosa mengi kwenye mchezo kwakua inaweza ikawa tatizo kwenye mchezo wa marudiano.
Kocha wa Yanga George Lwandamina aliwatoa Deus Kaseke na Haruna Niyonzima nafasizao zikachukuliwa na Donald Ngoma na Emanuel Martine.
Kwaupande wa Kocha wa Mc Alger aliwatoa Goveri Kaled, Nekkache Hichem na Bougueche Hajj nafasi zao wakaingia Awady Said, Feedab Zahir na Seguer Mohammed.
KAMUSOKO AIPA USHINDI YANGA DHIDI YA WA ALGERIA
Title: KAMUSOKO AIPA USHINDI YANGA DHIDI YA WA ALGERIA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Yanga imeibuka na usindi wa bao moja dhidi ya MC Alger katika mchezo wa kombe la Shirikiso Afrika uliofanyika kwenye uwanja wa tai...
Post a Comment