SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: SIMBA YAENDELEA KUJIFUA KUWAKABILI WANA NKURUKUMBI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Utasema nini kama sio shauku na dhamira kubwa yakuona walichokifuata Bukoba wanafanikiwa kukipata? Timu ya Simba iliyowasili jana mchana...
Utasema nini kama sio shauku na dhamira kubwa yakuona walichokifuata Bukoba wanafanikiwa kukipata?

Timu ya Simba iliyowasili jana mchana mjini Bukoba mkoani Kagera. Asubuhi ya leo wameonekana wakijifua vilivyo katika uwanja wa Mtungamo nje kidogo ya mji wa Bukoba.

Simba wanaonekana kuwa na ari kubwa wakiwa kwenye maandalizi ya kuwavaa Kagera Sugar, asubuhi ya leo wamefanya mazoezi ya nguvu kujiweka tayari kwa kukabiliana na Wanankurukumbi hao.  Mchezo utakaovurumishwa tarehe 2 mwezi wa nne katika uwanja wa Kaitaba Bukoba.

Kwa hali ilivyo katika msimamo wa ligi kuu, kila mchezo sasa ni mhimu kwa kila timu. Kagera Sugar wanahitaji ushindi ili waingie katika tatu bora na Simba wao ni vita ya ubingwa wakichuana kwa karibu na watani wao wa jadi Young Africans maarufu kama Yanga.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top