Timu ya soka ya Simba sc imeendeleza wimbi la ushindi baada ya kuifunga timu ya Mtibwa Sugar kwa magoli 2-0 katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa katika uwanja wa Uhuru leo hii.
Mpaka mapumziko matokeo yalikuwa 0-0, Kipindi cha
pili kilianza kwa kasi sana huku timu ya Simba ikifanikiwa kupata goli la
kwanza kupitia mshambuliaji wake Ibrahim Ajibu aliyeunganisha kwa kichwa kona
iliyopiga na Shizya Kichuya katika dakika ya 52.
Goli la pili la Simba lilifungwa na Laudit Mavugo
kwa shuti kali sana baada ya kupokea pasi ya Mwinyi Kazimoto. Mpaka mwamuzi
Raphael Adong'o kutoka mkoa wa Mara akipuliza kipinga cha mwisho matokeo
yalikuwa wa goli 2-0.
Post a Comment