Kocha Mkuu wa timu ya Taifa
ya Mpira wa Miguu ya Ufukweni, John Mwansasu amemuita Kipa wa Mbeya City ya
Mbeya, Juma Kaseja Juma kuongeza nguvu kwenye kikosi chake kinachotarajia
kusafiri kwenda Abidjan kucheza na wapinzani wao Ivory Coast kwenye mchezo wa marudiano
wa kuwania nafasi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika.
Kaseja mwenyewe, amefurahia wito
huo na wakati wowote anatajiwa kujiunga na kambi hiyo iliyopo kwenye Hosteli za
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume,
Ilala jijini Dar es Salaam.
Mwansasu amesema kwamba
Kaseja anaweza kumsaidia kwenye kikosi chake kwa kuwa mbiu za mchezo huo,
nafasi ya kipa inaweza kuamua matokeo kutokana na kuwa na uwezo mkubwa wa
kutengeneza timu ya mafanikio hivyo amemuita kwenda kusaidiana na Ahamed Rajab.
Nyota wengine wanaounda kikosi
hicho ni Talib Ame, Ahamada Ahamd, Mohammed Makame, Ahamed Rajab (golikipa)
Khamis Said, Yacob Mohamed Ally Raby, Mwalimu Akida, Khalifa Mgaya, Rolland
Revocatus, Juma Sultan, Rajab Ghana, Samwel Salonge, Kashiru Salum, Juma Juma
na Kevin Baraka.
Tanzania inatarajiwa kuondoka
Septemba 14, mwaka huu kwenda jijini Abidjan, Ivory Coast ambako timu hizo
zinacheza mchezo huo wa mwisho huko Ivory Coast na mshindi wa jumla atakuwa
amefanikiwa kufuzu kwa fainali.
Itakumbukwa kwamba kwenye mchezo
wa kwanza uliofanyika Agosti 26, 2016 hapa Dar es Salaam, Tanzania ililala kwa
mabao 7-3 katika mchezo ambao ulichezeshwa na waamuzi kutoka Uganda ambao ni
Shafic Mugerwa atakayepuliza kipyenga na wasaidizi wake ni Ivan Bayige Kintu na
Muhammad Ssenteza wakati Mtunza muda alikuwa Adil Ouchker wa Morocco na
Kamishna akiwa ni Reverien Ndikuriyo wa Burundi.
Post a Comment