Na Saleh Ally
SIMBA
ilishuka uwanjani kucheza mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons ya
Mbeya. Mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jiji Dar es Salaam
ni ya 23 kwake.
Wakati Simba imecheza mechi ya 23, Azam FC inaendelea kubaki na mechi 20 wakati Yanga imecheza mechi 21 tu.
Rnk | Team | MP | W | D | L | GF | GA | +/- | Pts | | ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
1 | Simba SC | 23 | 17 | 3 | 3 | 41 | 13 | 28 | 54 | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
2 | Young Africans | 21 | 15 | 5 | 1 | 51 | 11 | 40 | 50 | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
3 | Azam | 20 | 14 | 5 | 1 | 36 | 13 | 23 | 47 | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
4 | Mtibwa Sugar | 21 | 11 | 6 | 4 | 26 | 14 | 12 | 39 | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
5 | Tanzania Prisons | 23 | 9 | 9 | 5 | 21 | 20 | 1 | 36 | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
6 | Mwadui | 23 | 9 | 7 | 7 | 22 | 19 | 3 | 34 | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
7 | Stand United | 22 | 9 | 3 | 10 | 19 | 20 | -1 | 30 | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
8 | Ndanda | 22 | 5 | 9 | 8 | 19 | 23 | -4 | 24 | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
9 | Mbeya City | 22 | 6 | 6 | 10 | 22 | 28 | -6 | 24 | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
10 | Majimaji | 23 | 6 | 6 | 11 | 13 | 32 | -19 | 24 | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
11 | Toto African | 22 | 5 | 8 | 9 | 19 | 30 | -11 | 23 | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
12 | Kagera Sugar | 23 | 5 | 7 | 11 | 17 | 25 | -8 | 22 | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
13 | JKT Ruvu | 23 | 5 | 6 | 12 | 23 | 37 | -14 | 21 | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
14 | Mgambo JKT | 23 | 4 | 8 | 11 | 18 | 28 | -10 | 20 | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
15 | Coastal Union | 23 | 4 | 7 | 12 | 14 | 29 | -15 | 19 | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
16 | African Sports | 22 | 4 | 5 | 13 | 7 | 26 | -19 | 17 |
Ukiangalia
timu ambazo zinashinda kileleni ni Simba, Yanga na Azam FC. Hizi mbili
za Azam na Yanga zinashiriki michuano ya kimataifa ya Caf. Huenda ndiyo
kigezo TFF wanataka kukitumia timu moja kuwa na viporo vya mechi tatu na
moja viporo vya mechi mbili.
Yanga
wakati wanarejea, watakuwa na mechi mbili kibindoni wakati Azam FC wana
mechi tatu ambazo hawajacheza. Hili suala limeanza kuzungumzwa takriban
wiki tatu zilizopita na TFF ilikuwa ikijikanyaga kutaka kuiangushia
mpira Bodi ya Ligi ambayo ilikiri TFF inahusika. Hili ni lile sakata la
kuiruhusu Azam FC kwenda kushiriki michuano kule Zambia na kuacha ligi
ikiendelea.
Kinachoonekana
hapa ni umakini wa chini kabisa wa TFF na Bodi ya Ligi katika suala la
upangaji wa ratiba kwa kuwa zinatengeneza mazingira kwa timu fulani kuwa
na nafasi ya kufanya inavyotaka, nitaeleza kwa nini.
Wakati
TFF inapanga ratiba, kawaida inakuwa inajua michuano yote ya Caf
inatakiwa kuchezwa lini. Ninamaanisha Ligi ya Mabingwa kwa Tanzania
wawakilishi ni Yanga na Kombe la Shirikisho ambalo tunawakilishwa na
Azam FC.
Kama
TFF inakuwa inajua, hakika si vibaya kuwepo kwa kiporo cha mechi moja.
Hii unaona inatokea hadi Ulaya. Lakini hakuwezi kuwa na mechi tatu kwa
timu moja haijacheza.
Mfano
kama Azam FC ina mechi tatu, vipi Yanga ina mechi mbili kibindoni? Bado
utaona wazi kabisa kuna hali ya uzembe au figisu na inawanyima haki
Simba na timu nyingine.
Utaona,
Azam FC imefikisha viporo vya mechi tatu, eti kwa kuwa ilitakiwa kwenda
Afrika Kusini mapema. Lakini Yanga ikacheza mechi moja kwanza halafu
ndiyo ikaondoka kwenda Kigali. Tofauti ya safari zao, Yanga inatumia
karibu saa mbili hadi Kigali, Azam FC inatumia saa tatu na dakika
ishirini. Kipi kilifanya Azam wasicheze mechi yao moja?
Lakini
vipi kwingine wanaweza na tofauti ya kiporo inakuwa ni moja tu! Vipi
hapa TFF inashindwa na hili ndilo tatizo kubwa linaloendekezwa na mwisho
litakuwa matatizo.
Timu
moja inapobakiza mechi nyingi mkononi, hii hujenga hisia ya hofu ya
kupangwa kwa matokeo. Hili limekuwa likihofiwa duniani kote, ndiyo maana
timu hutakiwa kucheza mechi kwa wakati mmoja ili kuliepusha.
Sisemi
Yanga au Azam wamepanga matokeo, lakini bado si haki kwao kuwa na mechi
tatu mkononi na hili hauwezi kuona linatokea katika nchi yoyote. Kwenye
nchi nyingine, wanaohusika na upangaji ratiba pamoja na wasimamizi wake
kama TFF, hauwezi kuona wanafanya kama inavyofanyika hapa nyumbani.
TFF
wanapaswa kuwa makini, kwani hali inavyokwenda wanaonekana kufanya
mambo mengi ya kubahatisha na bahati mbaya wanakuwa na uhusiano mwingine
nje ya ligi, jambo ambalo linaweza kupelekea hisia ambazo si sahihi.
Kwamba wanaipendelea Azam FC kwa kuwa kampuni yao nyingine inadhamini
ligi.
Mimi
niende moja kwa moja bila ya kona, kwamba wanachofanya TFF katika suala
la ratiba si sawa, ni ubabaishaji wa mambo na wanapaswa kujipanga
vizuri.
Natuma
salamu zangu tena kwa Mkurugenzi wa Mashindano wa TFF, kwamba katika
kipindi chake mambo yanazidi kwenda shaghalabaghala na hili niliwahi
kuzungumzwa kuhusiana na uwezo wake kwa maana ya kuwa na uzoefu mdogo
kabisa katika nafasi hiyo, akakasirika.
Lakini
sasa mambo yanafeli yeye akiwa dereva, hivyo lazima akubali kwamba
anapaswa kubadilika. La sivyo, hisia za timu fulani zinatengenezewa
mazingira ya ubingwa, haziwezi kuisha na mwisho zitazaa ukweli.
Post a Comment