SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: SIMBA WAMUOMBEA AFYA NJEMA KIPA WAKE WA ZAMANI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Klabu ya Simba imepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya mchezaji wake wa zamani Abel Dhaira ambae amepata ugonjwa wa kansa ya tumbo. Dhair...
Klabu ya Simba imepokea kwa mshtuko mkubwa taarifa ya mchezaji wake wa zamani Abel Dhaira ambae amepata ugonjwa wa kansa ya tumbo.
Dhaira ambae ni golikipa wa zamani wa timu ya taifa ya Uganda na anayechezea klabu ya IBV Vestmannaeyiar ya Iceland alipata kuichezea klabu yetu ya Simba kwa mafanikio makubwa miaka michache iliopita.
Klabu imepokea taarifa za ugonjwa huo kwa taharuki kubwa na inaungana na Dhaira na familia yake kwenye kipindi hiki kigumu cha maradhi hayo makubwa

Tunaamini licha ya matibabu atakayoyapata kipa huyo pia nguvu ya Mwenyezi Mungu inahitajika katika kumponyesha nyota wetu mahiri Abel Dhaira.

Mungu ampe Afya njema Abel na Kumrudishia uzima wake.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top