Kiingilio cha chini cha mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za
Mataifa Afrika kwa Wanawake kati ya timu ya Taifa ya Tanzania ya
Wanawake ‘Taifa Stars’ dhidi ya timu ya taifa ya wanawake Zimbambwe
kitakua shilingi elfu mbili tu.
Mchezo huo namba 3, unatarajiwa kuchezwa siku ya Ijumaa saa 10 kamili
jioni katika uwanja wa Azam Complex uliopo Chamazi, huku kiingilio cha
juu kikiwa shilingi elfu tatu kwa jukwaa kuuu.
Waamuzi wa mchezo huo ni Lidya Tafesse, akisaidiwa na Yehuzewdubizua
Yehuw, Tsige Sisay, Woinshetkassaye Abera kutoka nchini Ethiopia, huku
Kamisaa wa mchezo huo Geneviev Kanjika akitoka Congo DR wote
wanatarajiwa kuwasili siku ya Alhamisi mchana kwa shirika la ndege la
Kenya (KQ).
Wakati huo huo kikosi cha Twiga Stars kimeendelea na mazoezi
kujiandaa na mchezo huo wa siku ya Ijumaa, huku kocha mkuu wa timu hiyo
Nasra Juma akisema vijana wake wote wapo katika hali nzuri na tayari
kuwakabili Wazimbambwe.
Aidha Kocha Nasra amewaomba wadau wa mpira wa miguu nchini na
watanzania wote kwa ujumla, kujitokeza uwanjani siku ya Ijumaa kuja
kuwapa sapoti katika mchezo huo, ambapo watakua wakiwakilisha na
kupeperusha bendera ya Tanzania.
KUZIONA TWIGA VS ZIMBABWE BUKU 2000 TU CHAMANZI
Title: KUZIONA TWIGA VS ZIMBABWE BUKU 2000 TU CHAMANZI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kiingilio cha chini cha mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa Afrika kwa Wanawake kati ya timu ya Taifa ya Tanzania ya Wanawake ...
Post a Comment