Mshindi wa mwezi wa Disemba, 2015 ni Ibrahim Ajib ambapo amepata kura
nyingi zaidi zilizopigwa na mashabiki na wapenzi wa Simba na soka wa
Tanzania kwa ujumla kupitia simu za mkononi ambao pia wamejiunga na
huduma ya Simba News.
Akikabidhiwa tunzo pamoja na pesa taslim Tsh 500,000/= na Mkuu wa
kitengo cha biashara na mipango kutoka EAG Group ambao ni washauri na
watekelezaji wa Masoko na Biashara wa Simba, Richard Mvula, Ibrahim Ajib
alisema “kila siku nimekuwa nikiendelea kujitahidi kufanya vizuri zaidi
ili nami ifike siku niweze kukabidhiwa tunzo hii, kwakweli ni heshima
kubwa sana kwangu, napenda kuchukua fursa hii kuupongeza uongozi mzima
wa Simba kwa kuanzisha utaratibu huu, pia napenda kuwashukuru mahsbiki
wangu ambao wamenipigia kura, wachezaji wenzangu kwenye kikosi cha Simba
ambao kila siku tumekuwa tukishirikiana katika kazi yetu hii ya mpira,
napenda kushukuru kwa sapoti kubwa ninayoipaa kutoka kwa familia yangu
na mwisho napenda kumshukuru Allah kwa kuendelea kunibariki na neema
zake kila siku”
Akimakabidhi tunzo hiyo Mkuu wa kitengo cha biashara na mipango
kutoka EAG Group Richard Mvula alisema “kama mtakumbuka utaratibu huu
ulianzishwa kwa ajili ya kuwapa motisha wachezaji wetu na sasa umekuwa
ni utamaduni wetu katika kuwapongeza na kuonesha kuthamini jitihada
zinazofanywa na wachezaji wetu katika kuutafuta ushindi wa msimu huu”
Napenda kuwakumbusha wanachama na wapenzi wa Simba kuendelea kuwapa
sapoti wachezaji wetu kwani kwa sapoti yao ndio mafanikio ya timu yetu
yanapopatikana, aliongeza Mkuu wa kitengo cha biashara na mipango kutoka
EAG Group Richard Mvula
Akizungumza jinsi tunzo ya mchezaji bora itakavyoendeshwa, Mkurugenzi
Mkuu wa EAG Group, Imani Kajula alisema “Wanachama na wapenzi wa Simba
na wapenda michezo ndio watakao kuwa wanachagua mchezaji bora wa mwezi
kwa kutuma jina la mchezaji wanayempendekeza kwenda kwenye namba 15460,
Ni wale tu ambao wamejiunga na Simba News kupitia mtandao wa Voda na
Tigo wataweza kupiga kura kuchagua mchezaji bora wa mwezi wa Simba”.
Tukumbuke kuwa unaweza kumchagua mchezaji bora wa mwezi ukiwa
umejiunganisha na huduma ya Simba News kwa kutuma jina la mchezaji
kwenda namba 15460. Zoezi la kumchagua mchezaji bora wa mwezi wa
Januari, 2016 litaanza February 29 2016. Piga kura mara nyingi zaidi
kuweza kumpata mchezaji wako bora wa Mwezi Januari, 2016.
AJIB AKABIDHIWA TUNZO YAKE YA DISEMBA
Title: AJIB AKABIDHIWA TUNZO YAKE YA DISEMBA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mshindi wa mwezi wa Disemba, 2015 ni Ibrahim Ajib ambapo amepata kura nyingi zaidi zilizopigwa na mashabiki na wapenzi wa Simba na soka wa ...
Post a Comment