Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limetangaza viingilio
vya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) Jumamosi kati ya watani wa jadi
Simba SC dhidi ya Yanga SC utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam, huku kiingilio cha chini kikiwa ni Shilingi elfu saba tu
(7,000).
Kiingilio cha juu cha mchezo huo kitakua shilingi Elfu Thelathini
(30,000) kwa VIP A, Elfu Ishirini (20,000) VIP B & C, Elfu Kumi
(10,000) kwa viti vya rangi ya machungwa (Orange), na Elfu Saba (7,000)
kwa viti vya rangi ya bluu na kijani.
Tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya Ijumaa saa 2 kamili
asubuhi katika vituo vya TFF (Karume), Buguruni Olicom, Ubungo Oilcom,
Kidongo Chekundu (Mnazi Mmoja), Posta (Agip), Dar Live (Mbagala), Uwanja
wa Taifa, Makumbusho Stand, Kivukoni Ferry.
Mchezo huo utachezeshwa na waamuzi wote wenye beji za FIFA, mwamuzi
wa katikati Jonesia Rukyaa (Kagera), akisaidiwa na Josephat Bulali
(Tanga), Samwel Mpenzu (Arusha), mwamuzi wa akiba Elly Sasii (Dar) huku
Kamisaa wa mchezo huo akiwa Khalid Bitebo (Mwanza).
KUZIONA SIMBA,YANGA BUKU SABA TU TAIFA
Title: KUZIONA SIMBA,YANGA BUKU SABA TU TAIFA
Author: Kalaghe Secondary School
Rating 5 of 5 Des:
Author: Kalaghe Secondary School
Rating 5 of 5 Des:
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) Jumamosi kati ya watani wa ...
viingilio vikubwa jamani walau wangeweka buku 5
ReplyDeleteviingilio vikubwa jamani walau wangeweka buku 5
ReplyDeleteHivi vimeshakuwa viingilio vyetu watani sasa tuwazoee tu tff
DeleteTuwazoee tu hawa Tifutifu na viingilio vyao. Ila huyu mwamuzi awe makini tu asituvugie soka
ReplyDeleteNin kweli kabisa Ndugu severine Machilla
DeleteUyo muamuz wao wakimleta longolongo kitawaka wallah.
DeleteKampa kampa tena.....! Shime shime tujazane mule! Maana uhakika wa kutapika ni mkubwa! Ajib, Mwinyi na hilo Kiiza.. aaaaaaargghh kampa....!
ReplyDeleteSimba nguvu moja tuiombe team yetu imfunge mtani
DeleteTunawafumua hawa vizurii tu
DeletePiga ao piga ao vyura fc
ReplyDeleteMambo ya kampa kampa tena, msimbaz kumenoga wa ndugu.
ReplyDeleteMwaka lazima wapoteane mambo ya kampa kampa tena kafinya kampa tena kaiombea kwa mbele, lazima wakimbiane wale
ReplyDeleteMwaka lazima wapoteane mambo ya kampa kampa tena kafinya kampa tena kaiombea kwa mbele, lazima wakimbiane wale
ReplyDeleteWatakaa tu
Delete