Kalaghe Secondary School Kalaghe Secondary School Author
Title: KUZIONA SIMBA,YANGA BUKU SABA TU TAIFA
Author: Kalaghe Secondary School
Rating 5 of 5 Des:
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) Jumamosi kati ya watani wa ...
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) leo limetangaza viingilio vya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) Jumamosi kati ya watani wa jadi Simba SC dhidi ya Yanga SC utakaochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, huku kiingilio cha chini kikiwa ni Shilingi elfu saba tu (7,000).
Kiingilio cha juu cha mchezo huo kitakua shilingi Elfu Thelathini (30,000) kwa VIP A, Elfu Ishirini (20,000) VIP B & C, Elfu Kumi (10,000) kwa viti vya rangi ya machungwa (Orange), na Elfu Saba (7,000) kwa viti vya rangi ya bluu na kijani.

Tiketi za mchezo huo zitaanza kuuzwa siku ya Ijumaa saa 2 kamili asubuhi katika vituo vya TFF (Karume), Buguruni Olicom, Ubungo Oilcom, Kidongo Chekundu (Mnazi Mmoja), Posta (Agip), Dar Live (Mbagala), Uwanja wa Taifa, Makumbusho Stand, Kivukoni Ferry.
Mchezo huo utachezeshwa na waamuzi wote wenye beji za FIFA, mwamuzi wa katikati Jonesia Rukyaa (Kagera), akisaidiwa na Josephat Bulali (Tanga), Samwel Mpenzu (Arusha), mwamuzi wa akiba Elly Sasii (Dar) huku Kamisaa wa mchezo huo akiwa Khalid Bitebo (Mwanza).

About Author

Advertisement

Post a Comment

  1. viingilio vikubwa jamani walau wangeweka buku 5

    ReplyDelete
  2. viingilio vikubwa jamani walau wangeweka buku 5

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hivi vimeshakuwa viingilio vyetu watani sasa tuwazoee tu tff

      Delete
  3. Tuwazoee tu hawa Tifutifu na viingilio vyao. Ila huyu mwamuzi awe makini tu asituvugie soka

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nin kweli kabisa Ndugu severine Machilla

      Delete
    2. Uyo muamuz wao wakimleta longolongo kitawaka wallah.

      Delete
  4. Kampa kampa tena.....! Shime shime tujazane mule! Maana uhakika wa kutapika ni mkubwa! Ajib, Mwinyi na hilo Kiiza.. aaaaaaargghh kampa....!

    ReplyDelete
  5. Mambo ya kampa kampa tena, msimbaz kumenoga wa ndugu.

    ReplyDelete
  6. Mwaka lazima wapoteane mambo ya kampa kampa tena kafinya kampa tena kaiombea kwa mbele, lazima wakimbiane wale

    ReplyDelete
  7. Mwaka lazima wapoteane mambo ya kampa kampa tena kafinya kampa tena kaiombea kwa mbele, lazima wakimbiane wale

    ReplyDelete

 
Top