Aliyekuwa kocha mkuu wa Simba sc Dylan kerr
ameitabiria ushindi timu yake ya zamani ya Simba sc dhidi ya Yanga katika
mchezo wa Ligi kuu ya Vodacom utakafanyika kesho katika uwanja wa taifa
Akizungumza na Simba damu fans blog, kocha kerr
alisema ni lazima simba ishinde mechi hiyo kwakuwa Simba wapo wanaongoza ligi.
Kerr alisema pia ni lazima Simba ashinde ili aweze kuwaacha mahasimu wa Yanga
kwa pointi 6."Katika mchezo wetu wa kwanza tulipocheza na Yanga ambapo
nilipoteza mechi ile,Tuliweza kuwashangaza sana Yanga, mechi ile tulitawala
mchezo wote. Vijana wangu waliweza kucheza mchezo mzuri sana na waliweza kupiga
pasi vizuri mno." Alisema Kerr. Kerr alisema pia naitakia Simba kila la
kheri katika pambano lao la kesho.
Mwisho Kerr alisema Nawamiss sana mashabiki wa
Simba,kila siku walifanya mimi niweze kuwa na furaha nyingi sana na ilikuwa
fahari kwangu kutembea mitaani na kuwaona mashabiki wa Simba wakiwa na furaha
sana"
Post a Comment