MAYANJA AWA KOCHAMSAIDIZI SIMBA
Jackson Mayanja aliyekuwa akiifundisha Coastal Union ya jijini Tanga leo ametua Simba kuwa msaidizi wa Dylan Kerr ambaye hakupata msaidizi tangu Seleman Matola ajiuzulu.
Mayanja ametua jana mchana na kuungana na kikosi cha Simba kilichopo visiwani Zanzibar ambako kinashiriki michuano ya Kombe la Mapinduzi na leo watacheza mechi ya nusu fainali dhidi ya Mtibwa Sugar.
Mayanja amewahi kuifundisha Kagera Sugar kwa mafanikio makubwa na tangu aondoke timu hiyo imekuwa ikisuasua kwenye ligi hata Coastal Union haijafanya vizuri ingawa sababu kubwa ni za kiutawala.
Post a Comment