Mwenyekiti wa timu ya soka ya Maji Maji fc, Humphrey Milanzi amethibisha ujio wa kocha mpya wa timu hiyo kuwa Kalimangonga ongala.
Milanzi amesema kuwa lengo kubwa la kumleta kally Ongala ni kuinusuru timu ambao ipo hati hati ya kushuka daraja. Kally ongala amesaini mkataba wa miezi 6 ambapo ataanza kukionoa rasmi kikosi hicho siku ya Jumanne. kally ongala amewahi pia kuchezea timu ya GIF Sundvall fc(Sweden), Yanga sc, Sinza fc na Bomu fc(zote za Tanzania). Timu nyingine alizocheza Kally Ongala ni Vasby united, Kajumulo fc na Seattle saints
Kwa upande wa Mshahara na posho za kocha, milanzi amesema kuwa ni wadhamini wa Symbion ndio watahusika na kumlipa kocha malipo yake. Ongala kwa sasa atashirikiana na Hassan Banyai kama kocha Msaidizi.
About Author

Advertisement

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Post a Comment