Kalaghe Secondary School Kalaghe Secondary School Author
Title: LIGI KUU TANZANIA BARA: SIMBA NA YANGA VIWANJANI KESHO
Author: Kalaghe Secondary School
Rating 5 of 5 Des:
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo saba kuchezwa katika viwanja tofauti, ikiwa katika mzunguk...
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara inatarajiwa kuendelea wikiendi hii kwa michezo saba kuchezwa katika viwanja tofauti, ikiwa katika mzunguko wa 16 kwa kila timu kusaka pointi 3 muhimu katika raundi hiyo ya lala salama.

Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam siku ya Jumamosi, Simba SC watawakaribisha African Sports, JKT Ruvu watawakaribisha Majimaji FC uwanja wa Karume, huku Mtibwa Sugar wakiwakaribisha Stand United kwenye uwanja wa Manungu, Turiani mkoani Morogoro.

Jijini Tanga, Wagosi wa Kaya Coastal Union watakua wenyeji wa Young Africans uwanja wa Mkwakwani, Mwadui FC watakua wenyeji wa Toto Africans uwanja wa Mwadui Complex, huku wakata miwa wa Kagera Sugar wakicheza dhidi ya Mbeya City katika uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top