Kikosi cha Simba leo tarehe 3
– 9 – 2015 kinatarajia kuwa na mchezo mwingine wa kirafiki na klabu ya KVZ
mchezo utakaofanyika saa 2 usiku katika uwanja wa Amani Zanzibar.
Kikosi
cha Simba kilichoweka kambi yake ya mazoezi visiwani Zanzibar chini ya kocha wake
mkuu Dylan Kerr pamoja wasaidizi wake kwenye benchi la ufundi, kimetaarifiwa
kuwa kipo salama na chenye ari ya ushindi katika msimu mpya ujao wa ligi kuu
Tanzania Bara 2015/2016.
“Wachezaji
wapo kwenye ari ya juu ya Ushindi na wanafanya mazoezi kwa bidii sana, sisi
kama benchi la ufundi tunasema kuwa wapenzi, wanachama na mashabiki wa Simba na
soka la Tanzania kwa ujumla wakae tayari kwa ushindani mkubwa utakaooneshwa na
kikosi chetu cha Simba”, Alisema Kocha Msaidizi wa Simba Suleiman Matola.


Post a Comment