Kalaghe Secondary School Kalaghe Secondary School Author
Title: COPA AMERICA 2015: MESSI AFIKISHA MECHI 100 ARGENTINA IKITINGA ROBO FAINALI COPA AMERICA
Author: Kalaghe Secondary School
Rating 5 of 5 Des:
+18 Messi akitafuta maarifa ya kuwatoka wachezaji wa Jamaica katika mchezo huo TIMU ya taifa ya Argentina imeibuka na us...


Messi is greeted by a wall of Jamaican defenders as Argentina look to double their advantage following Higuain's early breakthrough 
Messi akitafuta maarifa ya kuwatoka wachezaji wa Jamaica katika mchezo huoTIMU ya taifa ya Argentina imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Jamaica usiku wa kuamkia leo katika mchezo wa Kundi B michuano ya Copa America inayoendelea nchini Chile. 
Shukrani kwake mfungaji wa bao hilo pekee, Gonzalo Higuain dakika ya 11 tu ya mchezo huo na sasa Argentina inakwenda Robo Fainali.
Jamaica ambayo haijashinda mchezo wowote katika kundi hilo, tayari imeaga michuano hiyo. Lionel Messi aliyetimiza mechi 100 timu ya taifa, sasa anaweza kukutana na Ecuador, Peru au Venezuela katika Robo Fainali.
Kikosi cha Argentina kilikuwa: Romero, Rojo, Garay, Demichelis, Zabaleta, Biglia, Pastore/Pereyra dk59, Mascherano, Higuain/Tevez dk72, Messi na Di Maria/Lamela dk84.
Jamaica: Miller, Hector/Taylor dk71, Morgan, Laing/Dawkins dk71, Brown/Barnes dk78, McAnuff, Watson, Austin, Mariappa, Lawrence na McCleary.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top