Kagera Sugar imevunja rekodi ya Simba kuchukua ubingwa bila kufungwa baada ya kuifunga bao mbele ya Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mchezo uliofanyika uwanja wa Taifa.
Mchezo huo ulitumika pia kukabidhiwa Simba ubingwa wa ligi ambao kabla ya mechi ya leo walikuwa hawajapoteza mchezo wowote.
Hata hivyo idara ya ulinzi ya Kagera iliyokuwa chini ya Juma Nyoso na Mohammed Fakhi ilicheza nidhamu ya hali ya juu na kufanikiwa kuwabana hadi mapunziko.
Mlinzi Salim Mbonde aliyeingia dakika ya 50 kuchukua nafasi ya Kotei alitolewa tena dakika 15 baadae kufuatia kupata maumivu ya mguu.
Edward Christopher ndiye aliyeipatia Kagera bao hilo kwa kichwa baada ya kumalizia mpira wa krosi wa Japhet Makalai.
Simba iliwapumzisha Nicholas Gyan, Kotei na Mbonde nafasi zao zikachukuliwa na Mzamiru Yassin na John Bocco.
Kwa upande wa Kagera iliwatoa Atupele Green, Ally Ramadhan na Japhery Kibaya na kuwaingiza Omary Daga, George Kavila na Paul Ngalyoma.
KAGERA YAVUNJA REKODI YA SIMBA MBELE YA JPM
Title: KAGERA YAVUNJA REKODI YA SIMBA MBELE YA JPM
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kagera Sugar imevunja rekodi ya Simba kuchukua ubingwa bila kufungwa baada ya kuifunga bao mbele ya Rais ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzani...
Post a Comment