CAF ilituma Wakaguzi wake nchini Mei 21 kukagua miundombinu ya viwanja vitakavyotumika, viwanja vya mazoezi, hospitali na barabara.
Michuano hiyo imepangwa kufanyika katika viwanja viwili ambavyo ni uwanja wa Taifa na Azam Complex.
Kiongozi wa timu ya Wakaguzi kutoka CAF, Junior Binyam ameishukuru na Shirikisho la mpira wa miguu (TFF) na Serikali kwa maandalizi waliyofanya kuelekea michuano.
"TFF na Serikali zimefanya kazi nzuri, kwa niaba ya CAF nichukue nafasi hii kuwapongeza, ukaguzi wa pili utafanyika baada ya ripoti hii ya kwanza kukamilika," alisema Binyam.
Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Leodiger Tenga |
Kwa niaba ya Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo, Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Leodiger Tenga amesema mashindano hayo yatakuwa mazuri na ya kusisimua kwa mujibu wa maandalizi watakayofanya.
"Serikali imejipanga vizuri kupokea michuano hii, juzi mlimsikia Rais wa nchi Dk. John Magufuli na Waziri Mkuu wakizungumzia kuhusu michuano hili wakionyesha tumejipanga vilivyo," alisema Tanga.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka Shirikisho la soka barani Ulaya (UEFA) Ever Pasquier amefurahishwa na ukarimu wa Watanzania katika maeneo yote waliotembelea tangu walipotua nchini Mei 21.
Post a Comment