Msuluhishi wa kisheria wa
sakata la madai ya Simba dhidi ya Young Africans hali kadhalika Mchezaji Hassan
Hamisi Ramadhani maarufu kama Hassan Kessy, Wakili Msomi, Mzee Said El-Maamry
anatarajiwa kukutana na pande zinazopingana Alhamisi Novemba 3, mwaka huu ili
kufikia mwafaka wa mwadai hayo.
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi
za Wachezaji iliagiza pande za Simba na Young Africans kumaliza suala hilo
mapema mwezi uliopita, lakini kwa sababu zilizo nje ya TFF na Kamati yake
walishindwa kufanya hivyo kupewa barua ya wito kuitwa kikaoni Oktoba 29, mwaka
huu.
Hata hivyo, msuluhishi huyo
alishindwa kuendelea na kikao hicho baada ya taarifa kutoka Young Africans
kusema kwamba mmoja wa Wawakilishi wake, Wakili Msomi Alex Mgongolwa kuwa
safarini Iringa alikokwenda kwa sababu ya matatizo ya kifamilia. Ilielezwa kuwa
Mgongolwa ambaye ni Mwanasheria wa Young Africans, alifiwa hivyo kuomba
kupangiwa siku nyingine.
Kutokana na hali hiyo, E-Maamry
amepanga sasa kukutana nna viongozi na/ au Wawakilishi wa pande zote mbili
Alhamisi saa 11.00 jioni kwenye ofisi za TFF ili kuketi chini ya kuangalia
namna ya kumaliza madai ya Simba iliyowasilisha mashauri mawili ambako moja ni
dhidi ya Young Africans ilihali jingine ni dhidi ya mchezaji Hassan Kessy.
Mzee El-Maamry amesema: “Ili
kutenda haki, lazima tutoe nafasi kwa pande zote kusikiliszwa. Ni vema
Mwanasheria wa Young Africans akasubiriwa.”
Kamati ya TFF inasuburi
makubaliano hayo, na ikitokea imeshindikana, suala hilo litarudi kwenye Kamati
hiyo kwa ajili ya uamuzi wa mwisho kwa mujibu wa taratibu, kanuni na sheria
zinazoongoza mpira wa miguu.
Post a Comment