Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara
'Vodacom' (VPL) inaendelea leo Alhamisi kwa mchezo mmoja kupigwa kwenye uwanja
wa Uhuru Dar es salaam.
Timu ya soka ya Simba ambao ndio vinara wa
ligi hiyo itakuwa mwenyeji wa Mbao FC ya Mwanza katika mchezo utakaopigwa jioni
ya leo. Mpaka sasa Simba ina
pointi 23 huku Mbao wakiwa na pointi 12.
Akizungumza na blog
hii Meneja Mkuu wa Simba Mussa Hassan amesema vijana wao wako katika ari nzuri
ya ushindi na wamejipanga kuibuka na ushindi na kuhakikisha wanapata point tatu
muhimu ili kujieka katika mazingira mazuri ya ubingwa.
Wamekuja wakati mbaya sana hawa Mbao, hakuna namna lazima wachapike tu...
ReplyDelete