SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: TAWI LA SDF LAIKARIBISHA 'SIMBA WEEK' KIAINA YAKE
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Wanachama  wa Simba tawi la SDF lenye makao makuu yake Tabata Kimanga, leo wameikaribisha wiki ya Simba kiaina yake kwa kwenda kufanya usa...
Wanachama  wa Simba tawi la SDF lenye makao makuu yake Tabata Kimanga, leo wameikaribisha wiki ya Simba kiaina yake kwa kwenda kufanya usafi katika Zahanati ya Tabata huku pia wakitoa msaada wa vifaa.

Akizungumza na mtandano huu mara baada ya kukamilika kwa zoezi hilo Afisa habari wa SDF, Ally Shatry 'Bab Chicharito'  alisema waliamua kufanya jambo hilo kwa sababu kuu tatu.


"Kwanza ni katika kutimiza wajibu wetu kwa jamii, pili ni kutimiza agizo la Rais John Magufuli kuwa kila jumamosi ya mwisho wa mwezi ni siku maalumu ya usafi lakini tatu ni kuikaribisha wiki ya Simba inayoanza rasmi kesho," alifafanua Bab Chicharito.

Misaada iliyotolewa na wanachama hao ni pamoja na sabuni ya unga na vipande, dawa za kuulia wadudu, fagio, maji ya kunywa, mikate na vifaa vingine vya kufanyia usafi.




kwa upande wake Dr Mtei aliyemwakilisha Mganga Mfawidhi alisema "nimeshangazwa sana na hiki kilichotokea, sijawahi kuona mtu yeyote au kikundi kikija hapa na kufanya haya mliyoyafanya, ahsanteni sana. Naamini wengine wakiona wataiga mfano huo."

SDF ni tawi la Simba lililozinduliwa na rasmi na Rais wa klabu hiyo Evance Aveva mwezi Oktoba mwaka jana lakini limekuwa moja ya matawi maarufu nchini kutokana na utaratibu wake wa kipekee katika uendeshaji.
  
BAADA YA KUWASILI ZAHANATI YA TABATA A  
BAADA YA KUWASIL KIKOSI KAZI KIKIPEANA MAJUKUMU

AFISA HABARI WA SDF AKIGAWA GLOVES KABLA YA USAFI KUANZA
KAZI IKIWA IMEANZA KUHAKIKISHA ZAHANATI YA TABATA A INAKUWA SAFI

KHALID MWINCHANDE AKIMWAGILIA SEHEMU YA BARAZA YA ZAHANATI

MOHAMED NAMMENGE MJUMBE KAMATI YA UTENDAJI AKIWAJIBIKA


MWENYEKITI KARIM BOIMANDA AKIMKABIDHI KILE WALICHOBARIKIWA TAWI LAO KWA MSIMAMIZI WA KITUO

BAADA YA USAFI WANACHAMA WAKAPOZI KWA PICHA YA PAMOJA

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top