Mshambuliaji wa kimataifa wa
Tanzania anayechezea timu ya Genk ya Ubelgiji, Mbwana Samatta anatarajiwa
kuungana na timu hiyo nchini Nigeria kwa ajili ya mchezo wa mwisho wa hatua ya
makundi kuwania nafasi ya kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON
2017).
Hadi mchana wa jana ni Kelvin Yondan pekee kutoka Young Africans ambaye hakuripoti kwenye
kikosi hicho kilichopiga kambi yake kwenye Hoteli ya Urban Rose iliyoko
katikati ya jiji la Dar es Salaam. Kipa mpya wa timu hiyo, Said Kipao alijiunga
na timu hiyo mara moja baada ya kuteuliwa na Kocha Mkuu, Charles Boniface
Mkwasa.
Taifa Stars inatarajiwa kwenda
Nigeria kwa ajili ya mchezo huo dhidi ya timu ya taifa ya nchi hiyo, Super
Eagles utakaofanyika Septemba 3, 2016. Licha ya mchezo huo kuwa sehemu ya
mchuano wa kuwania nafasi ya kucheza fainali hizo za AFCON 2017 huko Gabon,
lakini utakuwa ni wa kukamilisha ratiba baada ya Misri kufuzu kutoka kundi G
ambalo mbali ya Nigeria na Tanzania, pia ilikuwako Chad ambayo iliyojitoa
katikati ya mashindano.
Post a Comment